KURA NA MAFURIKO WAPI NA WAPI ?
Leo asubuhi kwenye daladala tukitokea Kivulini kwetu kuja mjini tulimsikia abiria mmoja akilalamikia lile agizo la watu wa mabondeni kuhama kutokana na kuwepo uwezekano mkubwa wa kukubwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazotarajia kunyesha muda wowote kuanzia sasa.
Jamaa huyu alikuwa akililalamikia lile tamko la kwamba safari hii atakayekaidi kuhama yakimkuta mafuriko hakutakuwa na msaada kama inavyokuwa miaka yote. Yeye alikuwa anasema kuhama hatahama na kwamba hayo mafuriko na yaje; ila anaisubiri kama ni hiyo serikali imnyime misaada kama ambavyo huwa wanapata miaka yote. Atakachofanya yeye ni kuhakikisha kuwa hapigii kura rasimu ya katiba iliyopendekezwa na hata uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani hatoshiriki. Huyu ndugu alikuwa anazungumza kwa hisia na hakuwa anatania.
Alipoulizwa ni kwanini hataki kuhama, yeye akasema katiba ya nchi inamruhusu yeye kama raia wengine kuishi popote anapotaka ili mradi havunji sheria. Na akaendelea kudai kuwa badala ya serikali kumboreshea makazi yake mahali alipo hapo bondeni inamhamisha kumpeleka ugenini huko Mabwepande wakati babu yake, baba yake na yeye mwenyewe wamezaliwa mjini Jangwani.
Alipoulizwa endapo mafuriko yatakuja na kumchukua akafa hiyo kura ya maoni na ya wabunge ataipigia wapi; akajibu kuwa kama kufa angeshakufa siku nyingi lakini amesalimika mafuriko yote tangu enzi leo afe kwa misingi ipi; kwa sababu serikali imesema ?
Huyu ni mmoja kati ya wakazi wengi wabishi ambao wamedhamiria kukaidi kuhama mabondeni. Kukaidi si tatizo. Tatizo ni hapo watakapoathirika na mafuriko na kuilazimisha serikali iwahudumie kwa ujeuri wao Maudhi zaidi ni ule msimamo wao wa kuwa lazima serikali iwahudumia kwa kuwa wao ni wapiga kura wa nchi hii.
Kivulini kwetu kwa hakika tumesikitishwa sana na ukaidi wa aina hii; wa mtu kufanya makusudi kuyatafuta matatizo na kulazimisha kutatuliwa matatizo kwa kisingizio cha katiba. Mtu wa aina hii hatofautiani sana na mtu anayekunywa sumu au kujinyonga kwa madai kuwa hawezi kufa na akifa basi siku zake zimefika. Watu hujiua faragha, lakini mbele za watu lazima binadamu waungwana watachukua hatua za kukuokoa, na wanapokuakoa huonyeshi kujali walichofanya kwa madai kuwa huo ulikuwa ni wajibu wao.
Hivi mpiga kura wa aina hii ni mgombea gani anayemtaka ? Lakini ajabu ni kuwa wapo wagombea wanaopenya mabondeni usiku na kuwaambia hao jamaa wapiga kura wao wasihame; kwamba wapo pamoja nao kwa lolote liwalo, na wasiwe na wasiwasi hata wakikubwa na mafuriko watahakikisha misaada kutoka serikalini inapatikana. Hizo ndiyo siasa za uchaguzi, kuomba kura juu ya maisha ya watu. Na je wapiga kura hao wakizama kabisa na kufa watawapelekea viroba vya maisha au uhai huko mochwari ili wafufuke waje kuwachagua.
Kivulini kwetu tulidhani ni wajibu wetu kuwafahamisha ndugu zetu mfahamu nini kinachoendelea. Mwaka huu ni wa uchaguzi na katika mafuriko yajayo lolote linaweza kutokea. Kama kweli tunawapenda wenzetu tuwasaidie sasa kwa angalau kuwashawishi na kuwasaidia wahame mabondeni ili tuwe nao salama hadi Oktoba mwaka huu tupate mchango wao. Isifike mahari tukawa na mashaka kuwa jeuri hii ni ya kufanya mafuriko kuwa mtaji wa kujikimu kimaisha wa kila mwaka kwa waathirika na mtaji wa kura kwa wagombea kwa kila kipindi cha uchaguzi. Lakini tujiulize wenyewe KURA NA MAFURIKO WAPI NA WAPI ?
Thursday, 19 March 2015
Wednesday, 18 March 2015
TUPIMIANE VIWANJA KILA MTU AFE NA CHAKE
Kama ilivyo ada Kivulini kwetu huwa hatukosi kero. Kero hizi huwa hatuzitafuti bali huwa zinatukumba kutokana na mazingira yenyewe yalivyo; mambo ya utandawazi, mambo ya tabia nchi, hali ya miundombinu na wakati mwingine ukosefu tu wa mirejeshonyuma juu ya masuala kadhaa ambayo tunadhani ni ya muhimu katika jamii yetu.
Safari hii tunaomba tuliweke wazi suala la viwanja ama ardhi katika ujumla wake. Tunaliweka wazi kwa sababu limeshakuwa tatizo na siku hadi siku linaendelea kukua kiasi kwamba limekuwa likisababisha majerudi na vifo kama ajali za barabarani.
Suala la ardhi halikutakiwa lifikie hapo kama kwa kweli nia ingelikuwepo ya kuondokana na adha hii. Inaelekea watu hawajali na pengine na serikali nayo imechukulia rahisi suala hili. Tunasema hivi kutokana na ukweli kwamba kuna migogoro mingine ingeliweza kutatuliwa bila hata ya gharama zozote zaidi ya maamuzi tu ya kuelekeza hawa waishi kule na wale waishi huku. Kwamba kutokana na maelekezo tu yasiyoeleweka kumetokea ugomvi katika baadhi ya maeneo kiasi cha kusababisha hasara za mali na upotevu wa viungo na maisha. Wakati mwingine tunafika mbali kwa kuwaza kuwa huenda ulegevu huu katika masuala ya ardhi wapo watu wananufaika ya migogoro hiyo.
Katika tatizo hili la ardhi kumekuwepo na maeneo ambayo wakati wa sehemu hizo kwa miaka nenda rudi wamepokonywa na maeneo hayo kugawiwa wengine kama wawekezaji na wakati mwingine si wawekezaji kitu. Unakuta ardhi ya kijiji kizima kinagawiwa mtu mmoja na kwa bahati mbaya sana mtu huyu kwa miaka kadhaa anakuwa hafanyi chochote katika eneo hili zaidi ya kuweka walinzi kuhakikisha mtu haingii eneo hilo. Usumbufu kwa wengi kwa ajili ya fahari ya mtu mmoja; taifa halifaidiki na jamii haifaidiki.
Yapo maeneo ambayo wananchi wamenyang'anywa bila ya majadiliano wala makubaliano. Wakihoji najibu yanakuwa ardhi ni mali ya serikali hivyo chochote kinaweza kufanyika. Lakini ni kweli haki kumpokonya ardhi mkazi wa siku nyingi na kuigawa ardhi hiyo bila ya kumweleza utaratibu utakuwaje baada hapo ? Huyu au hawa walishajenga nyumba zao, walishapanda mimea yao ya kudumu, walishajipangia maisha yao hapo. Wakitoka hapo waende wakavamie wapi ili maisha yaendelee; huko ambako tafrani kama hii iliyowakumba haitawakumba ? Wakati mwingine jinsi wanavyoondolewa katika maeneo yao nyumba huchomwa moto au kubomolewa.
Kuna maeneo wananchi wanavamiana. Wafugaji wanawavamia wakulima. Wakulima wanafyeka mashamba maeneo ya wafugaji. Hakuna mipaka, hakuna utaratibu, hakuna sheria ila ni kila mtu na ubavu wake; mwisho wa siku eneo linakuwa halilimiki wala halifugiki; kila siku vilio.
Wote tunajua kuwa Watanzania wa leo wanalenga kila mtu kuwa na makazi yake. Miji inapanuka; Dar es salaam inakutana na Kibaha n.k. Watu wanauziana mashamba, mashamba yanakuwa makazi. Lakini viwanja havipimwi, ujenzi unaendelea holela; hakuna maeneo ya wazi, hakuna barabara, hakuna huduma; kila mtu kwa uwezo wake. Mjini humo kuna wanaofuga nguruwe, ng'ombe na mbuzi. Mjini humo kuna wenye viwanda vya kuranda mbao, kusindika mafuta, kusaga viungo vya pilau na viwanda vya gongo. Mjini humo humo kuna kumbi za kukesha za disko, kuna bar jirani na shule, misikiti mkabala na makanisa n.k Haya mambo yamejengwa holela; hayafungamani, hayatangamani na mpangilio wake tu ni kero.
Ukija uswazi huku ndiko maisha magumu. Choo mlangoni kwa jirani. Gari unaliacha mtaa wa pili, barabara haipo zaidi ya uchochoro. Ukitokea msiba hakuna mahali pa kupitisha jeneza, inabidi mwili ubebwe hadi mtaa wa pili ndipo upambwe. Watoto hawana pa kucheza, na ukitokea moto mtaa huo kunakuwa hakuna jinsi zaidi ya kuupigia makofi moto uteketeze nyumba salama.
Maisha kuhusiana na viwanja ama ardhi kwa ujumla ni kero. Tusichokielewa Kivulini kwetu ni kwanini iwe hivyo. Inakuwa hivyo kwa faida ya nani. Na itakuwa hivyo hadi lini.
Kinachojitokeza ni kutokuwepo na mipango mahususi ya upimaji wa viwanja, ugawaji wa viwanja na urasimu mwingi katika kutoa hati za viwanja; kwa ujumla suala la viwanja na ardhi limejaa urasimu kiasi kwamba kwa mtu wa kawaida linatia kizunguzungu.
Kivulini kwetu tunauliza, ni kwanini kama wizara inaona suala hili limewazidi kimo shughuli hii ya upimaji wasiibinafsishe. Tunaziuliza mamlaka zenye wakazi wenye shughuli zinazokinzana kama vile wafugaji na wakulima kwanini wasitengewe maeneo kwa uwazi na uhakika ili kila mtu ajue mipaka yake ili kuondokana na hali hii ya sasa na kutumishiana misuri.
Na hawa wawekezaji mwitu wanaopewa ardhi maekali kwa maekali tena yenye rutuba lakini hawayafanyii chochote kwa miaka nenda rudi na kuwaacha wakazi katika maeneo makame wanaachiwa kuendelea kumiliki maeneo hayo ?
Kivulini kwetu tunashauri serikali itupimie kila mtu na eneo lake, apewe hati yake aishi kwa amani. Ipime na igawe maeneo kwa kila kijiji ili kijue mipaka yake. Wakulima waelekezwe maeneo yao, wafugaji weaonyeshwe maeneo yao. TUPIMIANE VIWANJA NA ARDHI YETU KILA MMOJA AFE NA CHAKE.

Tuesday, 17 March 2015
BAYA MOJA HUFUTA MEMA MENGI
Leo Kivulini kwetu tulikuwa na mjadala wa kijamii juu ya tabia inayoambatana na msemo wa BAYA MOJA HUFUTA MEMA MENGI. Sambamba na kujadili tabia hiyo tukawa pia tunajiuliza ni kwa nini kwa manufaa ya jamii tusingelibadili tabia na kufuata usemi wa JEMA MOJA HUFUTA MABAYA MENGI.
Katika kuiangalia jamii yetu tumekuta tabia hii imekuwa ikimuathiri kila mmoja wetu katika maeneo na nyakati tofauti.
Utakuta mtu ni mfanyakazi katika ofisi fulani. Pengine huyu ndugu kwa miaka zaidi ya kumi ya utumishi amekuwa akifanya kazi zake vizuri kwa uaminifu na unyenyekevu.Na si hivyo tu, pengine ni mbunifu na ameliingizia shirika au kampuni mamilioni ya fedha kwa kiaka nenda rudi. Siku moja baada ya miaka 10 akatokea kufanya kosa, pengine la upotevu wa kiasi kidogo sana cha fedha ama uzembe wa kusababisha hasara ya kiasi kidogo sana cha fedha; kinachotokea ni kuwa uongozi au utawala bila kuzingatia mchango wake wa kiaka kumi watamtimua kazini na wakati mwingine kumdhalilisha mpaka kwenye vyombo vya habari; hivi ni kweli kampuni haiwezi kuheshimu mema na mazuri aliyofanya mtumishi huyu kwa kipindi chote cha utumishi wake ? Hivi mfanyakazi bora kwa miaka mitatu mfurulizo katika kampuni anaweza kuchukuliwa sawa na mfanyakazi mwingine ambaye hajawahi kuchukua tuzo yoyote mahali pa kazi ?
Utakuta kijana kasomeshwa na familia na hatimae kapata kazi. Baada ya kuwa kazini akawa si mchoyo kwa kujitahidi kumsaidia kila ndugu atakayekuja kuomba msaada kwake. Ndugu watasaidiwa na watamsifu kutokana na wema wake. Baada ya muda kijana wao atakuwa na familia na hivyo majukumu yake kuongezeka na kubadilika. Kidogo kidogo ataanza kushindwa kutoa misaada kama awali na pengine kushindwa kabisa kuacha familia yake ili asaidie ndugu. Hapo sasa ndipo ndugu wataanza kuja juu kuwa kijana wao toka ameoa amebadilika sana. Na hawataishia hapo bali watamwita mpumbavu kwa kuwasaidia wakwe zake badala ya wazazi wake; watasema mkewe au mmewe kamroga ili asisaidie familia yake n.k Kisa wamekwenda kuomba wakakosa kupewa.
Utakuta katika chama cha siasa kuna wanachama ambao wamefanya kazi kubwa sana katika kukijenga chama; wakati mwingine walilazimika kutoa mali zao ili chama kisitetereke. Wapo waliouza utu wao na kuhatarisha maisha yao ili kuhakikisha chama kinasonga mbele. Lakini siku wanahoji chochote katika chama, viongozi bila kujali mchango wao na haki yao ya msingi katika chama watawatengenezea zengwe na kuwafukuza katika chama.
Utakuta katika Klabu ya soka mchezaji amekuwa ndiyo tegemeo. Mchezaji huyo pengine ndiye aliyechangia kuipandisha daraja timu; ama ndiye aliyekuwa msaada mkubwa kuhakikisha timu haishuki daraja; ama ndiye mfungaji hodari kiasi cha timu kunyakua ubingwa mara kadhaa. Yeye kama binadamu anaweza kukosea ama wakati mwingine kwa kumdhania tu kuwa ameuza timu; klabu huuvunja mkataba wake ama kumfikisha mahakamani kwa sababu hii au ile na kusahau kabisa mangapi alifanya kwa manufaa kwa klabu.
Utakuta mume au mke amekuwa mwaminifu katika ndoa kwa kipindi cha miaka chungu nzima lakini ikatokea siku akachepuka, basi hiyo kesi haitaisha na hakutakuwa na msamaha mpaka na ndoa inavunjika; kisa ni kosa la siku moja ndani ya uaminifu wa miaka hata zaidi ya ishirini.
Kivulini kwetu tuliibua mifano mingi sana ya athari za tabia hii ya kufuta wema wote kwa ubaya wa siku moja na kujiuliza hivi sisi wanajamii tabia hii itatusaidia nini; ni kwanini tumekuwa wepesi wa kusahau mema na kutoa maamuzi makali hata pale tunapohakikisha kuwa hili ni kosa la kwanza. Ni kwanini hatui wavumilivu; kwanini hatupeani ushauri nasaha; kwanini hatusameheani zaidi badala yake tunakuwa wepesi wa kuhukumiana. Kwa taarifa ya mjadala huu tuna imani wengi watakaosoma watatafakari ya kuchukua hatua.
Thursday, 5 March 2015
SAFARI YA KUTOKA UZALENDO WA KAWAIDA KWENDA UASI KUPITIA UZALENDO CHOTARA
Kilio chetu ni juu ya zile harakati za kutusafirisha bila ya ridhaa yetu kutoka kwenye Uzalendo halisi wa nchi yetu kutupeleka kwenye Uzalendo Mwitu au Uasi kwa jina jingine dhidi ya nchi yetu.
Japo tumechelewa kutafakari lakini ni heri tumejitahidi kuliwaza hilo wakati tayari tumekwisha fikishwa katika Uzalendo Chotara.
Wataalamu wanasema siku zote ukiweka viumbe wawili wenye asili moja iwe ni mmea au mnyama na wakakaa kwa kipindi fulani, cha kwanza kutokea huwa ni kiumbe chotara na baadae kiumbe cha asili mojawapo.
Tunaamini kuwa yeyote anayejichanganya kimaongezi mitaani na katika mitandao atakubaliana na sisi kuwa kauli, mawazo na mtizamo wa wananchi wengi kwa sasa unaashiria ukomavu wa Uzalendo Chotara; yaani mawazo na mtizamo wa wananchi kutoridhishwa na mwenendo mzima wa nchi yao, wananchi kutowapenda viongozi wao, wananchi kulalamikia karibu kila jambo, Uzalendo wa kubeza, kukejeri, na kulaani kila jambo. Kauli za utengano, kauli za dharau, na kauli za vitisho. Kuna kauli nyingi sana ambazo hatukuzoea kuzisikia katika nchi yetu sasa hivi zimekuwa ni za hawaida; watu hawaoni haya wala hawaoni vibaya.
Kivulini kwetu tumebaini kuwa kustawi kwa uzalendo huu chotara hakukuja kama ajali; tunaamini kabisa uzalendo huu ulitokana na mchanganyiko wa Uzalendo halisi na Uzalendo mwitu. Watu waliudaka Uzalendo mwitu katika upya wake wakidhani kuwa huo ndio ustaarabu. Kwamba ili uonekane msomi mzuri basi uwe na kifua cha kuisema serikali na kukashifu nchi; kwamba ili uonekane tajiri basi shurti uwakashifu wananchi na uwakejeri viongozi; kwamba ili uonekane umetembea sana duniani, basi uweze kuponda mambo ya kwetu na kuimba mambo ya ughaibuni; kwamba ili uonekane mtu makini ni lazima uchote fedha za umma na uhujumu nchi; Tuliingia mkenge kupitia utandawazi tukajiona tumepata na kumbe tumepatikana.
Hapo mwanzo ilikuwa ni aibu mtu kusimama na kujidai kuwa ana shamba ekari 2000 Mpanda; au ana maroli 90 ya kusafirisha mafuta ama ana vijisenti kama dola 20 milioni Uswisi kwani ni kiasi ambacho kilikuwa kikivuta hisia ya utovu wa Uzalendo. Sasa hivi hata wanafunzi wanaweza kuwa na mali; nani atawauliza ? Nakumbuka enzi ya Sokoine mtu kuonekana na bidhaa kiasi fulani; haikuwa na haja ya mamlaka kumfuatilia bali yeye mwenyewe kwa jinsi alivyolelewa alikuwa anaona aibu. Waswahili wana sema kawaida ni kama sheria. Watu kama Sokoine hawakumbukwi kwa ukorofi wala sura zao bali wanakumbvukwa kwa Uzalendo wao.
Tumefika mahali ambapo Uzalendo Chotara huo unaanza kututafuna. Tulianza kwa kulia kizaire kwa kutumia magitaa sasa hivi tunalazimika kulia kwa midomo na machozi machoni. Tumechoka na mvurugano wa mawazo, tumechoshwa na msongamano wa itikadi na tumechanganyikiwa na hekaheka za falsafa kila uchao. Tunaamini yapo mazuri na tunaamini pia yapo mabaya lakini kuyapambanua inatupa shida kutokana na kupigiwa makelele kila uchao na magwiji wa Uzalendo Mwitu. Sasa hivi wao ndio wanaojua kila kitu na wanatulazimisha na sisi tufanye watakavyo. Haiwezekani.
Tunadhani ni wakati muafaka kuelezana haya ili kukusanya nguvu tuweze kuachana na safari hii mbaya. Ikiwa hapa tu katikati tulipofika hali imekuwa mbaya kiasi hiki je tukizidi kuendelea huko itakuwaje ? Tunadhani ule Uzalendo tuliouacha nyuma ndio mali kuliko huo Uzalendo Mwitu tunaoufuata. Kama maendeleo ndiyo haya ni heri turudi nyuma kwani hata tukiyapata maendeleo hayo hayatusaidii; sana sana yatatuacha tukiwa mahututi na taabani.
Wednesday, 4 March 2015
NINA MASHAKA SANA NA KUNDI HILI LA VIJANA
Jana jioni Kivulini kwetu tulikuwa na mjadala juu ya kundi la vijana. Kundi tulilokuwa tukiliongelea ni kundi la vijana wasomi na wasiosoma, wadogo kwa wakubwa lakini ambao wapowapo hawana mbele wala nyuma. Kundi hili ni la vijana waliomaliza shule au vyuo lakini hawana la kufanya na ni kundi linalojumuisha vijana wenye afya na uwezo wa kufanya kazi. Hili ni kundi linalokula kwa kengere makwao ama kundi linalozagaa kujidonyolea mitaani na usiku kulala kwenye magofu, upenuni mwa nyumba, kando ya barabara ama kukesha wakinywa viroba, kubwia unga au kuvuta bangi waweze kupoteza mawazo.
Kivulini kwetu tulilifananisha kundi hili na nyasi kavu msimu wa kiangazi; nyasi ambazo akitokea mlevi akatupa kichungi kisichozimwa juu yake; moto utakaolipuka hapo kuuzima ni majaliwa yake mola. Kundi hili tulilifananisha ya sinia la dagaa wabichi wazima linaloelea ziwani ambapo yakitokea mawimbi wakati wowote hutakuwa na kitu katika sinia bali matone ya maji kwani wote wakakuwa wameishia ndani ya maji.
Kundi hili la vijana ni kubwa na siku hadi siku linaendelea kukua katika miji yetu. Tumekuwa na vijana wengi ambao mchana kutwa wanashinda wamejiinamia, wanawaza, kufikiri na kupanga mipango ambayo hatuijui ni ipi na kwa hakika hatujui hatma yao itakuwaje.Kundi la vijana wenye hasira na chuki kwa nchi yao. Vijana ambao wako tayari hata kumtafuna na kummeza mbaya wao endapo wataonyeshwa kwa kidole kuwa huyo ndiye anayewasababishia matatizo waliyo nayo.
Hawa ni watoto wetu, jirani zetu, shemeji zetu na kwa kila hali wanatuhusu. Kwa kuwa wanatuhusu ni wajibu wetu kujua wanaishije; kwa maana ya kuwa tujue wanakula nini na wapi, wanalala wapi na wanamudu vipi kuzipata japo hizo huduma japo ni duni. Tunapaswa tujiridhishe na uhalali wa maisha yao kabla makubwa hayajatukuta.
Kivulini kwetu tulifanya tathmini ya haraka na kubaini kuwa zipo familia nyingi ambazo baba au mama ama baba na mama wana jukumu la kulisha ndugu wasiopungua sita ambao wapo tu hapo nyumbani kwao wakiwa hawana kazi yoyote kutwa nzima zaidi ya kuangalia TV na kuwapokea wenye nyumba vifurushi warudipo nyumbani.
Tulikwenda mbali zaidi na kubaini kuwa katika hali halisi ya kipato cha Mtanzania wa kawaida, mshara wake unamtosha kula yeye na mkewe tu na pengine usiwafikishe mwisho wa mwezi. Kufika hapo tukajiuliza kama ndivyo wanafamilia hawa wanamudu vipi kuwahudumia hawa ndugu wa ziada katika familia zao; tena kwa kipato cha halali.?
Tumekuta ni wachache sana wenye vijimradi ambavyo vinawapunguzia makali kwa kipato zaidi kujazia mshahara lakini kundi kubwa tukaanza kulishuku kuwa linaendesha maisha kiaina. Linaendesha maisha kwa kukopa, kuiba, kutapeli, na kula rushwa makazini kwao na mitaani. Ikiwa mahitaji ni 700,000/= kwa mwezi na kipato ni 300,000/=; unaweza kujitahidi kuziba pengo kwa mwezi mmoja lakini kwa mwaka ni lazima uingie msituni ukasake nyoka; ukatapeli, ukakope, ama ukapokee rushwa. Na kadri majukumu yanavyoongezeka katika familia na utapeli, rushwa, wizi na ukopaji pia unaongezeka. Hii kitaifa ni hatari kuwa sana.
Mada yetu kuu haikuwa athari za kifamilia zinazoletwa na vijana hawa bali tulikuwa tukijitahidi kukuna vichwa juu ya nini tufanye ili kupunguza joto linaloletwa na vijana hawa kwa sababu mateja wamo katika kundi hili, panya rodi wamo katika kundi hili, waandamanaji wa kukodi wapo katika kundi hili, vibaka, machangudoa, wapiga debe, watoto wa mitaani, ombaomba, na wengine wengi ambao mbali na kuwa mzigo kwa jamii wamekuwa tishio la usalama na amani katika taifa letu.Hawa wako tayari kuunga mkono chochote kiwe cha halali ama hatari ili mradi wahakikishiwe kuwa watapata kitu. Kwa bahati mbaya kundi hili limekuwa likitumiwa kwa maasi zaidi ya mambo mema; kulipwa kidogo na kicha kuachwa wakiwa na majeraha ya mwilini na mioyoni.
Kivulini kwetu tunasikitishwa na kuongezeka kwa kundi hili katika nchi yenye ardhi kubwa na nzuri, nchi yenye madini mengi, nchi yenye wanyama wa kila aina, na nchi yenye amani na utulivu. Miji yetu ina kazi nyingi za kufanya na wafanyaji wengi wanazagaa lakini tumeshindwa kabisa kuunganisha kazi na wafanya kazi ili tuweze kuondoa aibu hii ili kundi hili litusaidie kusonga mbele kimaendeleo.
Mfano mdogo usio na gharama; tukienda mjini Dar es salaam kumejaa takataka kila mtaa, wakazi wa mitaa wanazichukia taka hizo na wanazo fedha za kuwalipa wazoaji taka; hapo hapo mjini ndiko kwenye vijana wengi wanaoshinda wakiranda bila ya kazi ya kufanya mpaka wanaishia kutapeli ama kuwachomoa watu mifukoni ili wapate pesa ya kununua chakula.
Kivulini kwetu tunajiuliza hivi wana Ustawi wa jamii wako wapi watusaidie mawazo juu ya kuwasaidia vijana wetu hawa ? Wizara husika wana mipango gani juu ya vijana hawa ? Umoja wa vijana wa kila Chama cha Siasa ni nini mchango wao kwa vijana hawa ambao ndio wapiga kura na wadau wao ? Mashirika ya Dini na madhehebu mbalimbali, zaidi ya nasaha mnawasaidia vipi vijana hawa. KUMBUKENI KUWA HAWA NDIYO NGUZO YA TAIFA; WAKIOZA HAWA NA TAIFA LITAKUWA LIMEOZA.
Mjadala huu bado haujafika mwisho. Kivulini kwetu kwa leo tutaishia hapa lakini tutaendelea nao ili tuhakikishe tumeridhishwa kuwa umeeleweka ipasavyo katika jamii yetu na hatua zinachukuliwa.

Monday, 2 March 2015
EBU FIKIRIA WEWE UNGELIKUWA ALBINO UNGEJISIKIAJE
Ndani ya hotuba hiyo kulikuwa na mambo kadhaa ambayo singelipenda nirarejee ila miongoni mwayo lilikuwepo suala ya Mauaji ya Albino(Ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi). Sipendi nirejee alichosema ila ningelipenda niliongee kwa namna nyingine; nia ikiwa ni kujaribu kuwasaidia wale ambao pengine hawakuweza kuelewa nini kilichokuwa kikisisitizwa katika hotuba ya Rais.
Nadhani wote tunakubali kuwa hayupo aliyebahatika kutoa maoni ama mapendekezo azaliwe vipi; hivi tulivyozaliwa tulijikuta tumezaliwa hivyo. Wapo watu ambao wangelipenda wazaliwe wanawake lakini kwa mapenzi yake mola wamejikuta wamezaliwa wanaume. Na wako wanaume ambao wangelipenda wazaliwe wanawake lakini bahati haikuwa yao badala yake wamezaliwa wanaume. Ni kwa mifano hiyo walioutaka ufupi wakapewa urefu, walioutaka weupe wakapewa weusi na kadharika na waliotaka wazaliwe kawaida wakazaliwa Albino. Na ndiyo sababu kila uchao binadamu hujifanyia marekebisho katika kazi ambayo mwenyezi mungu aliifanya bila ridhaa yake ili angalau kuifurahisha nafsi yake. Tumeshuhudia wanaume wakisuka nywele na kuvaa bangili na mikufu ili angalau wafanane na wanawake; tumeshuhudia akina mama wakijichubua kutoa rangi nyeusi wawe weupe na kuvaa nywele za singa wawe kama wazungu au waarabu; tumeshuhudia wafupi wakivaa viatu vya mchuchumio waonekane angalau warefu kidogo; tumeshuhudia wembamba wakinywa dawa za "kichina" wawe wanene; na mengine mengi. Lakini katika madawa yote sijaisikia dawa ya kumfanya Albino awe na ngozi ya kawaida; pengine wangeliweza kubadili ngozi zao ili kujisalimisha na wauaji hawa.
Kwa kuwa hayupo hata Albino mmoja aliyeomba azaliwe hivyo bali wamezaliwa kwa mapenzi yake mola. Mimi au wewe tungweliweza kuzaliwa Albino kwa sababu tunajua hatukushiriki kujichagulia rangi ya kuzaliwa nayo. Sasa kwa ukweli huo hii jeuri ya kwanza kuwanyanyapaa Albino inatoka wapi na hii imani ya kuwa Albino wanavuta mafanikio inatoka wapi. Rais kauliza jana kuwa kama imani hiyo ina ukweli wowote kwanini basi hao Albino wakiwa mwili kamili hawakuwa mamilionea ila wakiwa vipandevipande wanaleta utajiri ?
Na iwe iwavyo, ni binadamu gani ambaye leo akiambiwa kuwa apoteze maisha yake ili japo watoto wake wapate utajiri atakuwa tayari; na hilo linakuwaje jepesi kwa wenzetu ?
Utaratibu wa kuwavamia na kuwacharanga kinyama Albino ni unyama ambao hauna lugha nzuri ya kuuelezea ukaeleweka katika uzito wake. Kwanza hawa wenzetu wanao upungufu katika kuzaliwa; kana kwamba hilo halitoshi tunawaongezea janga jingine la kuwaua; hii ni laana ambayo kama hatukuifanyia kazi italiangamiza taifa letu. Tunajisikiaje kusoma habari zao magazetini, kuziona katika TV; kwamba leo mmoja kacharangwa kule, kesho mwingine kauawa huku na tunatikisa miguu kana kwamba tunaangalia mechi ya Simba na Yanga ama Filamu ya King Majuto; hatuoni haya wala hatusikii vibaya. Ipo sinema moja ilikuwa ikionyesha ukatili huo wanaofanyiwa Albino; binasfi sikuweza kuiangalia hadi kufika robo; inatisha.
Ebu kila mtu ajifikilie na yeye angelikuwa Albino; anasikia habari za Albino wenzake wanavyouawa; na yeye anakuwa akitembea akijua wakati wowote atavamiwa na kunyofolewa kiungo chochote; hajui aende wapi akajifiche na kwa nini afanye hivyo; ana makosa gani katika dunia hii. Jamani tumwogope mungu. Kama hiyo ndiyo namna ya kutajirika ebu tufikirie namna nyingine; vinginevyo tukubali kubaki maskini kuliko kuwa matajiri juu ya damu za watu tena watu wenyewe walemavu wa ngozi. Ukiendesha gari la kifahari, ukienda kutalii Dubai, ukila kuku, ukinywa bia; mwenyewe unajisifu kuwa imetokana na mkono au mguu wa Albino. Kama ndivyo wewe ni shetani aliye hai ambaye huna haki na kuchanganyika na binadamu wa kawaida. Na ulaaniwe ufe mapema tena ufe kinywa kikiwa wazi kama ishara ya ubaya ulioutenda duniani kwa hao watakaoihudumia maiti yako.
Kitaifa hii ni vita; na iwe vita ya kila mmoja wetu kuhakikisha kila fununu juu ya vitendo hivi inafanyiwa kazi. Walio karibu na waganguzi wawe makini nao na wazifuatilie nyenendo zao ili kuweza kubaini kama wanahusika na chochote juu ya mauaji haya. Ma Albino tuwalinde popote walipo; tusiwatenge bali tuambatane nao ili angalau wapate imani kuwa jamii ipo nao. EBU KILA MMOJA WETU AFIKIRIE KAMA ANGELIKUWA ALBINO KWA MAISHA HAYA ANGELIJISIKIAJE.
RASIMU IWE MBAYA AU NZURI KUIPIGIA KURA NI MUHIMU.
Moja ya majukumu ambayo yako mbele yatu katika Taifa letu ni kura ya maoni ya kuikubali au kuikataa rasimu ya Katiba mpya inayopendekezwa. Hili ni jukumu muhimu, nyeti na haki ya kila mwananchi mwenye sifa za kupiga kura.
Mchakato wa kuiandaa Rasimu hii umechukua muda mrefu na umegharimu kiasi kikubwa cha fedha za wananchi. Ili kuweza kupima matunda ya kazi iliyofanyika ni jambo la busara kwa wananchi kukamilisha hatua muhimu ya kuipigia kura rasimu hii ili kuweza kujua ni kipi kitaendelea baada ya hapo.
Kivulini kwetu tunatoa maoni haya dhidi ya mawazo mengine ya watu wengine ambao wanashawishi zoezi la kupiga kura ya maoni juu ya Katiba mpya lisifanyike. Wao nao wanazo sababu zao ambazo kwa mtazamo wao wanadhani ni za muhimu.
Sisi tofauti na wao nadhani kufanya hivyo ni kutukwaza, kutuchelewesha, na kutuyumbisha; kwa sababu kama suala ni uhalali wa mchakato, ushirikishwaji duni au kuburuzana yote hayo yanajibiwa na kura ya hapana. Na kama zoezi ni halali, haki ilitendeka, na katiba ni nzuri basi yote hayo yanajibiwa na kura ya ndiyo. Kwa kutoa haki pande zote suala la kuipigia kura rasimu ya katiba ni muhimu.
Kivulini kwetu hatukutaka tuseme; labda kwa kulazimishwa, kuwa mshindani huwa haleti vikwazo na hagomi kuingia ulingoni isipokuwa pale tu ambapo huwa ana mashaka na ushindi wake.
Kama hukuingia ulingoni kujipima uwezo wako ni lini basi utakuwa na uhakika na kiwango chako ?Kama hatupiga kura kuikubali au kuikata Rasimu hii ni njia gani sahihi itatuhakikishia kuwa Rasimu hii ni mbaya au nzuri; tukisie tu !; na kwanini tuandikie mate ilhali wino tunao ?
?
Nilidhani kila mmoja wetu atajitahidi kuwaelimisha anaowadhani hawaelewi ubaya, uzuri, mapungufu, na makunjufu ya katiba ili kumweka kila mwananchi katika ufahamu wa kumwezesha kuamua apige kura ipi siku itakapowadia kuipigia kura Rasimu ya Katiba.
Tunasema hivi kwa sababu hatuelewi nini kitafuata endapo rasimu hiyo haitapigiwa kura........mchakato utaanza upya ?, ama zoezi hilo litasitishwa na iwe basi, au itakuwaje ? Na je muda na gharama zilizotumika itakuwa ndiyo basi tena ama vipi ? Na kauli ya nani itakuwa kipimo cha kufikia maamuzi ya kutopiga kura ? Kwa sababu taratibu na kanuni zilizopo zinaelekeza kura ipigwe.
Bado hatujakubali kuwa hata kama kila kitu tunachosema hakikuzingatiwa kingelizingatiwa; Katiba hiyo isingelikuwa na mawazo yote tuliyonayo, bado tungelihitaji kupata fulsa nyingine wakati mwingine kuipitia tena na kurekebisha hapa na pale kulingana na mahitaji na muda utakaokuwepo. Sasa basi kwanini tusiipigie kura Rasimu hii kwanza tukajihakikishia kuwa ni kwa kiasi gani tunaikataa ama kuikubali ili hata kama tunaingia hasara basi tuwe wote tumeikubali kwa sababu ambazo wengi wamezikubali.
Ushauri wetu ni kwa kila mmoja wetu kujikita katika kutoa elimu juu ya Rasimu hii na kumwandaa mwenzake au kujiandaa yeye kuipigia kura Rasimu ya Katiba ili tuweze kuingia katika hatua inayofuata kwa amani bila ya makelele wala fujo.
Subscribe to:
Posts (Atom)